Hii ni filamu ya Maua Arts Group iliyotengenezwa na SHP MEDIA. Ni Story iliyomuhusu kijana Stephan kumpenda kwa dhati mtoto wa kitajiri aitwaye Jesca,Lakini mapenzi yanapoanza kushamiri mama yake na Jesca anagundua na kutengenisha uhusiano huo kwa kutumia silaha ya moto,je nini kitaendelea kaa chonjo imeshatoka jikoni
Friday, July 31, 2009
KILIO CHA WANA MAUA ARTS GROUP
Ndugu wafadhili sisi ni vijana tusiopenda kwenda mtaani na kufanya uhalifu,tumejikusanya na kuunda kikundi kinachofaamika na BASATA na tumekuwa tukifanya matamasha mbali mbali pamoja na kwenye kampain za serikalini.
Kwa dhati toka miyoyoni mwetu tunahitaji msaada wenu ili tuweze kujiendesha kulingana na mipangilio tuliyonayo mbele yetu.
Sio kwamba tumejiunga ili tuweze kuomba msaada bali kwa hakika sisi ni vijana tunaojituma kupambana na changamoto za kimaisha,ndio maana tumekuwa tukijichanga changa mpaka kufanikisha kutengeneza FILAMU YA KIBONGO IITWAYO STEPHAN.
Filamu imeshakamilika na sasa tunatafuta msambazaji mwaminifu wa kusambaza kazi yetu
Macho yetu ni kwa kwako wewe unayeweza kutusaidia kwa namna moja au nyingine Please Tunakutegemea. Waweza kuwasiliana nasi kwa kutumia njia zetu za mawasiliano zilizopo hapo juu mkono wako wa kushoto.Thanks.
Filamu imeshakamilika na sasa tunatafuta msambazaji mwaminifu wa kusambaza kazi yetu
Macho yetu ni kwa kwako wewe unayeweza kutusaidia kwa namna moja au nyingine Please Tunakutegemea. Waweza kuwasiliana nasi kwa kutumia njia zetu za mawasiliano zilizopo hapo juu mkono wako wa kushoto.Thanks.
KARIBUNI WADAUUUUUUUUUUUU
Mhhh Wadau karibuni sana katika Blog yetu tulio izindua hivi karibuni,Sisi Wana maua tumeamua kufungua njia hii kutokana na maswali mengi toka kwa wadau wetu, ili jamii ituelewe zaidi imetulazimu kuweka mambo yote hazarani.
Kwa kutembelea blog yetu utafahamu mambo megi tuyafanyayo,Pia utaona jinsi tunavyowajibika juu ya jamii yetu nzima iliyotuzunguka, Najua utafikiri tunasema mambo mazuri kupendezesha blog yetu la hasha :-
- Tunawajibika kwa kufundisha sanaa kwa jamii iliyotuzunguka. Hapa tunawalenga wale watu wenye kupenda kwa dhati sanaa,na ambao watakubali kukaa sehemu moja kujifunza (tunajali sana kazi ndio maana tunaheshimu muda,kulinda wasanii wetu wasiharibu kazi zao) Kwa kufanya hivi tunakuza vipaji vya jamii iliyotuzunguka na kwa namna moja au nyingine tunawafufulia njia nyingine ya kutengeneza fedha
- Tunaelimisha jamii kuepukana na mauvu,kwa kufanya matamasha mbali mbali kwa kupinga,kuonya na kukemea utumiaji wa madawa ya kulevya,starehe za ngono zembe nk. Kutoa njia mbadala jinsi kuepukana na maovu hayo pia kuwasaidia waliothirika wa madawa ya kulevya na maradhi ya ngono zembe kwa kuwashauri na kuwaleta kwenye kikundi chetu kwa nia ya kuwafanya wawe busy na wawe katikati ya watu walioelimika na wenye mawazo positive.nk
- Kikundi chetu kina watu wenye fani mbali mbali wako wanyabiashara,wasomi degree level,Watu waliobobea kwenye fani ya Hotel management nk ndio maana tunaposema ni sehemu ya watu wenye hasira na maisha tunamaanisha
Subscribe to:
Posts (Atom)