Friday, July 31, 2009

KILIO CHA WANA MAUA ARTS GROUP


Ndugu wafadhili sisi ni vijana tusiopenda kwenda mtaani na kufanya uhalifu,tumejikusanya na kuunda kikundi kinachofaamika na BASATA na tumekuwa tukifanya matamasha mbali mbali pamoja na kwenye kampain za serikalini.

Kwa dhati toka miyoyoni mwetu tunahitaji msaada wenu ili tuweze kujiendesha kulingana na mipangilio tuliyonayo mbele yetu.

Sio kwamba tumejiunga ili tuweze kuomba msaada bali kwa hakika sisi ni vijana tunaojituma kupambana na changamoto za kimaisha,ndio maana tumekuwa tukijichanga changa mpaka kufanikisha kutengeneza FILAMU YA KIBONGO IITWAYO STEPHAN.
Filamu imeshakamilika na sasa tunatafuta msambazaji mwaminifu wa kusambaza kazi yetu
Macho yetu ni kwa kwako wewe unayeweza kutusaidia kwa namna moja au nyingine Please Tunakutegemea. Waweza kuwasiliana nasi kwa kutumia njia zetu za mawasiliano zilizopo hapo juu mkono wako wa kushoto.Thanks.


No comments:

Post a Comment